HUWEZI KUWA TAJIRI KWA KUBETI

 Unaweza kufilisika ndani ya masaa kwa kufanya mchezo wa kubeti.

Hii ni hatari kwa afya yako pia.


Siku hizi kumezuka michezo mingi sana katika jamii inayoitwa kubeti kwa lugha nyepesi ni mchezo wa bahati na sibu.

Mchezo huu huchezwa na watu wa rika zote hasa vijana na watu wazima ili waweze kujipatia kipato wengine wakiwa na ndoto za kuwa matajiri hapa duniani kwa njia hii.

Lakini kwa bahati nzuri au mbaya Leo napenda kukuambia tu wazi kabisa ni ngumu sana kuwa tajiri kwa kubeti ila unaweza kuwa kuchaa kwa kubeti. Maana kama mtu una 50,000/= halafu unadanganywa na makampuni uweke dau ubeti hiyo hamsini elfu halafu inaliwa basi hii hakuna tofauti na kichaa.

Leo hii wachina kila kona wameweka mashine za kubetia wanaita bonanza,  Leo hii wachina,wahindi na wabongo pia wamekodisha majumba kwa ajili ya watu kubeti hii ni hatari sana kwa uchumi wa vijana. Kiukweli vijana wengi sana wamekuwa na uraibu wa mchezo huu wa kubeti.

Kubeti haiwezi kumtajirisha mtu bali humfanya kuwa masikini zaidi hata kama alikuwa na umasikini nafuu kwa sababu unaweza ukawa na pesa nyingi sana lakini ndani ya dakika chache ukawa ombaomba ndugu yangu. Betini ni ukichaa fulani ambapo mwathirika yupo tayari kuhatarisha Mali zake kwa kubeti.

Kuna makala niilisoma mwezi wa sita mwaka huu juu ya dada mmoja wa Canada na kaka mmoja kutoka nchi ya Uganda; Mambo yalikuwa hivi;

Dada wa Canada alijinyonga kwa sababu alikuwa na madeni ya zaidi ya 100milioni yaliyozalishwa na zoezi la kubeti,  huyu dada aliuza nyumba ya mama yake aliyekuwa na umri wa miaka 65 wala pesa haikutosha kulipa madeni yote badaye akajinyonga akamwacha mama yake duniani hana pa kuishi maana nyumba imeshauzwa.

Kaka wa Uganda yeye alikuwa anauza bidhaa za boss wake kwenye Duka  siku hiyo aliuza 2.4milioni akashawishika kuweka dawa la pesa yote ya mauzo, mkeka ulikuwa na odd 2 hivyo alitarajia apate 4.8 million ili aondoke na 2.4 milion. Matokeo yake mkeka ulichana na aliomba magoli mawili tu kila timu yakaishia goli moja.baada ya mkeka kuchana kaka huyu alifadhaika sana na kuwaza atamwambiaje boss wake aliamua kwenda chumbani akajinyonga kwa kamba safari yake ya kusaka utajiri kwa njia ya kubeti ikaishia hapo.

Rafiki yangu njia hii ni mbaya mno ina madhara makubwa sana ni heri ukatafuta utajiri kwa njia nyingine kabisa, makampuni haya yanakusanya pesa nyingi sana kwa watanzania wasio na hatia. Kijana utakuta anaweka shillings 1000 akitarajia kupata 10,000,000 kwa kweli hizi ni ndoto za mchana kabisa.

Njia hii pia inaweza kukusababishia msongo wa mawazo hata kupata shinikizo la damu usipofanya maamuzi ya haraka kuacha kabisaa kazi hii. Nasikitika sana kuona vijana wanakaa katika majumba yenye mashine tangu asubuhi wakifanya kazi ya kubashiri timu zitakazoshinda kwa kweli huu ni utumwa

 kabisa. 




Madhara makubwa ya kubeti;

1. Muhusika kuendelaea kuwa masikini  kwa sababu ni biashara isiyo kuwa na uhakika kuwa utapata.

2. Kusababisha uraibu, yaani mtu anakuwa kama mlevi wa dawa za kulevya; 

3.Husababisha msongo wa mawazo.

4. Kusababisha umasikini katika taifa; kwa sababu vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa wanasubiria pesa ambayo hawana uhakika kama wataopata.

Kumbuka kuwa pesa unayotumia kubeti ungeitunza kwenye kibubu baada ya mwaka ungekuwa na mtaji mkubwa sana , lakini rafiki yangu umeamua kuwapa wachina na makampuni ya kibongo ili uwafanye watoboe maisha wewe unabaki kuwa chini tu siku zote.

Chukulia mfano; unacheza 1000 na inaliwa mara 5 utakuwa umetumia 5000 zidisha mara 30 ni sawa na 150,000 zidisha kwa 12 ni sawa na 1,800,000/= halafu wewe umepelekea watu watoke maisha , amka rafiki yangu utakuja kufa masikini.  Angalia sasa 1.8mil imeenda kwa mchina na wengine wengi tu maana siku hizi kuna utitiri wa makampuni ya kubeti na mlengwa ni wewe kijana.

Nakushauri achana kabisa na kubeti.

Nakuambia unaweza ukawa na pesa lakini ndani ya dakika 90 ukawa ombaomba.

Be careful my friend don't bet you will cry one day.


Be blessed. 

+255 763 826 410

Email  lmakelemo@yahoo.com

mkmconsultingservice@gmail.com



1 Comments

Previous Post Next Post