SIRI YA KUFANIKIWA KATIKA BIASHARA


Nitazungumza kipaumbele kikubwa kwa mfanyabiashara yoyote hapa duniani  akikifanya hata kama biashara yake ilikuwa karibu kufa itafufuka kwa spidi kubwa sana. 
Je unataka kukijua kipaumbele hicho? Basi fuatana nami katika makala hii:

Wafanyabiashara wengi sana hawaijui siri hii laiti kama wangeijua biashara zao zisingeanguka kabisa.  Siri hii ni kubwa sana washauri wengi hutoa ushauri wa kifedha na na rasilmali watu n.k lakini siri hii imeachwa nakutupwa nje kabisa kana kwamba ni kitu ambacho hakina maana yoyote.

SIRI hiyo ni; kumpa kipaumbele mfanyakazi wako uliyemwajiri.
Siri hii ni kubwa mno na ya muhimu sana,kwani wafanyabiashara wengi wapo tayari kuthamini majengo, Mali walizo nazo ila siyo watumishi.

Lakin ukiangalia hii ni  kukosa ufahamu wa kutosha juu ya biaahara kwasababu anayesababisha biashara yako iendelee ni mfanyakazi wako,bila kuajiri watu wakukusaidia huwezi kamwe kuendesha shughuli za biashara rafiki yangu.

Wafanyabiashara wengi hulalamika kuhusu mauzo na mwenendo wa biashara zao lakini kamwe huwezi kuwakuta wanaulizia changamoto za wafanyakazi wao ambao ndiyo injini ya uendeshaji wa taasisi zao. Mfanyakazi yupo hapo kwako ili akusaidie kutimiza maono yako kwa hiyo ukimfanya kuwa sehemu ya umiliki wa biashara yako ndugu utatoboa haraka sana.katika biashara yako lakini usipomfanya kama sehemu ya umiliki wa taasisi yako itachukua muda mrefu sana kupasua anga katika ulimwengu wa biashara.

1. Jali hisia za wafanyakazi wako
2. Walipe vizuri wafanyakazi wako
3. Wape muda wa kupumzika
4. Wape pongezi panapohitajika
5. Walipe kwa wakati kama utachelewa kulipa kwa sababu maalumu tafadhali wape taarifa mapema wajiandae kisaikolojia. 

Mfanyakazi akitimiziwa haki zake na akawa na furaha moyoni mwake ataifanya biashara yako kama yake.

Jitahidi kuwathamini wafanyakazi wako kwani bila wao huwezi kuendesha biashara peke yako.
Kuna baadhi ya wakurungezi huwafokea wafanyakazi wao na kuwaambia "mnajua nilivyoihangaikia biashara hii" ni kweli hawezi kujua maana hawakuwepo wakati unaanza, lakini waheshimu na kama kuna maswala ya kinidhamu fuata utaratibu wa kisheria.





Fanya haya ili ufanikiwe kwenye biashara yako rafiki yangu.

Taasisi yetu pia inatoa mafunzo na semina kwa wafanyakazi ili kuwajengea uwezo wa kujitambua kuwa wao pia ni sehemu ya umiliki wa taasisi wanayofanyia kazi.

Pia tuatengenza mifumo ya uendeshaji wa taasisi mbalimabli  kama vile:

1  kuandaa sera ya uendeshaji wa kifedha [ accounting policy]
2. Sera ya rasilmali watu. [Human resources policy]

Kwa ushauri wa kibiashara wasiliana nasi kwa;
Mobile: +255 763 826 410
WhatsApp +255 653 552 236

Email address: lmakelemo@yahoo.com makelemoconsultingservices79@gmail.com 

Ofisi zetu zipo 
Nyegezi karibu stand ya Mabasi
Mwanza.





Post a Comment

Previous Post Next Post