KUZA BIASHARA YAKO BILA MKOPO

 



Kuna watu wengi hapa duniani wanamsemo kuwa huwezi kuendesha biashara bila kukopa kwenye taasisi za fedha au kwa mtu binafisi. 

Mimi napingana kabisa na kauli hii, nasema kuwa inawezekana kuwa na biashara ndogo kabisa na ikakua mpaka kufikia millionaire bila kugusa mkopo wowote!. Tatizo wengi wetu tunapenda sana kuonekana kuwa tuna biashara kubwa ambayo mtu akifika anasema duh! Umejaza duka. 

Miaka zaidi ya 10 iliyopita nilizungumza na dada mmoja mchaga pale Dar es Salaam mazungumzo yetu yalikuwa hivi;

Lushinge; Dada kwa nini nyinyi wachaga mna maendeleo sana?

Dada: Sisi tabia zetu huwa ni kuanza kidogo kidogo ili taratibu unaanza kupanda juu mpaka unafikia mafanikio makubwa.

Kwa kweli nilijifunza jambo kubwa sana kwenye jibu la huyu dada, maana watu wengi sana wanatabia ya kutaka kuanza na mitaji mikubwa na wakati uwezo wao ni mdogo. Utakuta mtu ana laki 5 au hata elfu 50,000 lakini bado anakuambia hana mtaji. Au mwingine utamkuta ana simu smartphone yenye thamani ya kati ya 100,000 hadi 500,000 bado anakuambia hana mtaji haya ni maajabu sana.Hapa tatizo litakuwa kwenye ufahamu rafiki yangu. 



Madhara ya kuanza biashara au kukuza biashara kwa mkopo;

1. Kukosa huru wa pesa yako unayoipata.

Unapokopa pesa kwa ajili ya kuanza au kukuza biashara yako hutakuwa na huru na pesa yako kamwe. Maana kila mauzo unayofanya lazima ukimbizane na marejesho na gharama zingine zipo palepale.Kwa sababu ile riba unayopeleka kwenye marejesho nado faida yako rafiki. Mimi sipo hapa kuharibu biashara za wenye kampuni za kukopesha,  ila najaribu kutoa elimu kwa wananchi wenzagu tuweze kujua nyuma ya shilingi juu ya swala la mikopo. Mfano unabiashara halafu unakopa milion moja ukajaza duka vizuri, unalipa deni na riba 1,100,000 kila mwezi kwa miezi 6 utakuwa umelipa riba ya 600,000 rafiki yangu.Umeona jinsi uchungu wa mikopo ulivyo?

Ikiwezekana swala la mkopo liwe ni uchaguzi wa mwisho kabisa, mikopo inatesa sana imeua ndoa nyingi sana na kuwaacha watoto kama yatima. Na wahanga wengi ni wamama  wenye biashara  ndogondogo  do wanaobebewa hadi masufuria ya kupikia kisa hawajarejesha mkopo hii ni hatari sana rafiki yangu.  Kuna watu wamepata shinikizo la damu na stroke kwa sababu ya madeni. Hakuna mtu anayedaiwa akawa na amani ya kweli labda amani ya mchongo.

Nachukia mikopo maana haijawahi kumnyanyua mtu kimaisha zadi ya kukupeleka chini,angalia mfano hapo juu, yaani unamtengenezea mtu pesa ndani ya miezi 6 umemtengenezea jamaa laki 6 n wakati hiyo ilitakiwa iwe faida yako ili uendelee kupanua biashara yako.

2. Unakuwa utumwani;

Madeni ni utumwa mbaya sana, hata katika maandiko kwa wakristo kwenye biblia inasema kuwa tajiri humtawala masikini naye akopaye ni mtumwa kwake akopeshaye. Unapokopa pesa kwa mtu au taasisi tayari unakuwa umeuza uhuru wako kwa yule mtu, hutakuwa na sauti kwake mpaka ulipe deni, na ndiyo maana waharifu wanapofungwa mpaka amalize malipo ya kifungo ndipo awe uhuru kama ni miaka 2 au mmoja mpaka uishe ndo awekwe huru.

Kataa kuanza au kukuza biashara kwa kukopa badala yake fanya hivi;

Mfano una mtaji wa 100,000/= usijaribu kuingia tamaa kwa kuangalia watu wengine au kukubali kushawishiwa na mtu juu ya kukopa.

Faida unayoipata hata kama ni 10,000 tenga 2000 weka akiba maalumu ya kupanua biashara yako badala ya kwenda kukopa.

Jifanye hiyo pesa utakayoweka akiba siyo ya kwako hata siku ukihitaji kuitumia kwa ajili ya kupanua biashara jikopeshe kama vile umeenda kwenye kampuni ya mkopo. 

Jifunze kuweka akiba kila faida unayoipata mwenye biashara nakuhakikishia hutaingia katika madeni kamwe na utakuwa na amani na furaha hapa duniani. Hakuna furaha na raha hapa duniani kuishi bila kudaiwa na mtu yoyote awe hai au amekufa.

Lakini sentensi hii wengi hawaipendi kabisa wao wanachoamini ni kwamba huwezi kuishi hapa duniani bila madeni. 

Mwisho kama unataka biashara yako ife anza kukopa pesa.na kama unataka biashara yako iwe kubwa sana na kuwa tishio epuka mikopo. 


Kwa Ushauri wa kibiashara, mafunzo, seminars wasiliana nasi kama ifuatavyo:

Mobile number; 0763 826 410 

WhatsApp   0653 552 236 lmakelemo@yahoo.com makelemoconsultingservices79@gmail.com 


Office zetu zipo Nyegezi karibu na stand ya mabasi

Mwanza 

Post a Comment

Previous Post Next Post