Katika jamii tunayoishi watu wanaofanikiwa kwa kiwango kikubwa katika maeneo mbalimabli ni wale wanaoweza kufanya mambo ya tofauti na jamii kabisa ambayo pia yanaonekana kuwa hayawezekani kufanyika.
Kuwa milionea kwa kawaida si jambo rahisi kama wengi wanavyodhani, kwani linahitaji mchakato na uthubutu wa kufanya mambo mapya ya tofauti kabisa, Katika jamii tuliyonayo imekuwa haina uwezo wa kubuni vitu vipya ambavyo ni adimu kwenye ambavyo ni rahisi kutengeneza kipato kikubwa.
Mfano;
2.Ajira: Watu wengi sana wamekaririshwa kuwa ukisoma mpaka chuo kikuu hatima yako ni kuajiriwa tu hii ni hali ya hatari sana kwa jamii. Watu wamekuwa hawana uwezo wa kubuni vitu vitakaowapelekea kuwa mamilionea katika kizazi hiki. Sina maana kuwa kuajiriwa ni vibaya ,lakini ukiangalia soko la ajira kwa sasa ni gumu sana mfano nafasi moja yaweza kutangazwa lakini barua za maombi ni zaidi ya 1,000. Nakumbuka miaka takribani kumi iliyopita kuna ajira zilitoka uhamiaji hapa Tanzania nafasi zilikuwa 70 waombaji walikuwa shortlisted ni 10,000 unadhani hiyo nafasi utaipata? Wataipata wateule tu, maana kama vile maandiko kwenye biblia yanasema waitwao ni wengi lakini wateule ni wachache. Siku ya usahili tulifanyia uwanja wa taifa yaani ungefika siku hiyo ungedhani kuna mechi ya simba na yanga maana watahiniwa walikuwa wengi sana wakigombania nafasi 70.
Inashangaza sana kuona mwanchuo amegraduate degree ya mambo ya kilimo halafu anakaa nyumbani mpaka anakonda anasubiria ajira,Real this is disease. Tanzania tuna aridhi ambayo hajatumika lakini bado mtu analia ,wazungu wanakuja kuwekeza kwenye kilimo hapa Tanzania halafu wazawa tunalia na kisingizio ni hakuna mtaji oho mara hakuna uhakika wa masoko, hizi ni sababu zisizo na mashiko kabisa.
Mwaka 2022 nilitembelea ofisi ya afisa biashara wa jiji la Mwanza kujifunza mambo ya biashara nilimuuliza maswali 2 tu;
A. Kwa nini serikali haisadii wananchi wake kudhibiti bei za mazao, maana mimi nilikuwa nikilima sana mazao hasa ya bustani ukipeleka sokoni unakutana na bei za ajabu sana mwisho wa siku unakula hasara kila awamu unayolima.
B. Nawezaje kuwa milionea kwa kilimo?
Majibu;
A. Tatizo wananchi hawana muda wa kuwaona wataalamu waliowekwa na serikali kusimamia.
Masoko ni mengi sana na ya uhakika katika mazao na mifugo tatizo wananchi pia hawataki kurasimisha shughuli zao kisheria ambavyo vinaweza kuwawezesha kuuza hata nchi za nje kwa urahisi. Akasema unaweza kuanza hata kwa kusajili jina la biashara na ukawa na nyaraka zote za umiliki hapo wanunuzi wa nje ya nchi ni rahisi sana kuwapata.
B. Kuwa na uthubutu; hili ni jambo la muhimu, huwezi ukatoboa katika maisha bila kujikana nafisi yako kwanza. Watu wengi wakianza jambo akikutana na changamoto ndogo tu anakata tamaa na kurudi nyuma kabisa, hii huwezi kupata maendeleo makubwa.
Akatoa mfano wa dada Khadija Jabir amabaye mpaka sasa ni milionea mkubwa kule Iringa kwa kilimo cha bustani lakini historia yake si rahisi alikotoka. Alipata hasara mara nyingi sana hadi akapata kusimama hadi Leo akiwa ni binti mdogo sana kwa umri.
Nawashauri wanachuo mliohitimu tafadhali usirudi nyumbani kwa wazee kuwapa mzigo jamani. Pambana buni kitu cha tofauti ufanye mambo yatabadilika kabisa. Ni fedheha kubwa kukaa nyumbani na kula chakula na kulipiwa bill na wazazi hii ni laana.
Mtu yoyote akifikisha umri wa miaka 18 kama siyo mwanafunzi lazima ajitegemee.
Ajira hakuna je mikono,miguu na kichwa vimekatwa?
Awamu nyingine nitazungumza namna ya kufanya mambo ta tofauti ili uwe milionea kwa kuangalia mifano mbalimbali.
Kwa Ushauri wa kibiashara na namna ya kurasimisha Biashara au shughuli unazofanya uweze kuuza zaida waliana na
Makelemo consulting services kwa mawasilano yafuatayo:
Simu; 0763 826 410
WhatsApp;0653 552 236
Email: lmakelemo@yahoo.com.
Tupo Mwanza Nyegezi