Lawama/ kumlaumu mtu ni ile hali ya mtu kuona kwamba jambo fulani halijaenda sawa kwa sababu ya mtu fulani. Katika maisha haya tunayoishi kamwe usijaribu kumlaumu mtu kama ndo chanzo cha kushindwa kwako hasa katika maswala ya maendeleo.
"You can't be a failure until you finds someone to blame " yaani "Huwezi ukashindwa katika maisha mpaka utafute mtu wa kumlaumu "
Kwanini watu wengi wanalaumu watu kama ndo chanzo cha matatizo yao?
Kwa sababu hawajawa watu wazima: kipimo cha mtu mzima ni uwezo wa kuchukua hatma ya maisha yake mikononi mwake.
"When you become an adult you take full responsibility of your future " yaani "ukiwa mtu mzima unapaswa kuwajibika kikamilifu".
Mara nyingi tumekuwa tukilaumu sana watu,taasisi au serikali kana kwamba ndo chanzo cha shida zetu; lakini siyo kweli ni ile hali ya kutofanya wajibu wetu tu ndo sababu kubwa.
Siri kubwa ya mafanikio hapa duniani katika eneo lolote ni kutokuwa na mtu wa kumlaumu,bali fanya sehemu yako kisha .mwambie Mungu asante kwa kuniwezesha.
Mfano; kuna kijana mmoja dodoma alikuwa anasomeshwa na kaka yake tangu kidato cha kwanza mpaka chuo kikuu.Yule kijana alufanikiwa kumaliza chuo na kupata degree ya uhasibu. Pindi anasoma kaka yake alimwahidi kuwa hatakosa ajira akimaliza tu chuo. Alipomaliza chuo mambo hayakuenda kama alivyotarajia.
Ajira hakutafutiwa kabisa na huyo mtu ingawa alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Huyo kijana alitumia nguvu kubwa sana kumlaumu huyu ndugu lakini hakuna kilichosaidia hata kidogo.
Siku alipojua siri hii ya "You can't be a failure until you find some one to blame" alianza kuichukua hatma ya maisha yake mikononi mwake, muda mfupi alipata ajira tena kwenye shirika la kimataifa. Akaendelea kubadilisha kampuni, na akafanikiwa sana mpaka sasa ana kampuni yake ni mkurugenzi.
Hivyo ndugu ukitaka ufeli maisha tafuta mtu wa kumlaumu. Muda unaotumika kulaumu mtu ni muda ambao wengine wanautumia kuimalisha mipango yao.
Don't blame anyone for your failure.
Asante ndugu;
0763826410