AJIRA NI MTAJI WA KUWA TAJIRI.



Watu wengi katika jamii huamini kuwa ajira ndiyo suluhisho la matatizo katika maisha yao,lakini tumeona katika jamii watu wengi walioajiriwa wana maisha ya kawaida sana  ulilingamisaha na watu walio na mirasi yao binafisi. 

Kwa ufahamu wangu ajira ni Ukanda wa faraja yaani "employment is the comfort zone " it makes the employee comfortable only for a short moment.

Ni vizur  kuichukulia ajira kama sehemu ya kusaidia kutimiza mono ya mmiliki na kujipanga au kuwekeza mradi nje ya ajira kwa ajili kukabiliana na mipango ya maisha pindi unapokuwa nje ya ajiara.

Watu wengi wamekuwa wakiishi maisha mafupi sana wanapokuwa nje ya ajura au kustaadu, hii ni kwa sababu walizoea kupokea mshahara kila mwisho wa mwezi  na kumemazwa na advance salary. 

Advance Salary ni kiasi  cha mshahara kinachotolewa na mwajiri ili kutatua tatizo  la mtumishi kwa wakati fulani na pindi mshahara unapotoka mwisho wa mwezi kiasi hicho kinakatwa kwenye ile jumla ya mshahara matokeo yake huyu mtu hatakuwa na furaha kamwe maana kila mshahara anaopkea kila mwezi hatukutana kamwe bali utakutana na kamanda fulani anayeitwa madeni. 

Ataenda hivyo mpaka umri wa kustafu au mkataba kuisha muda wake halafu ana madeni  na pension akiipata atatumia kujenga na kula na kununua usafir  ndo wengi hufanya hivyo, hakika nakwambia mtu huyu hachukui round anapata ugonjwa wa moyo na kufa kwa sababu wakati huo hakuna cha advance salary. 

Ushauri wangu ni heri mtu ajiwekee malengo  kuwa atafanya kazi ya kuajiriwa kwa muda maalumu halafu anaanza kujitegemea akiwa na nguvu za kuweza kuhimili mikiki  mikiki ya mitaani.

Mfano kama .mshahara wako ni 300,000 take home.weka 50,000 akiba kila mwezi kwa mwaka utakuwa na 600,000/= ukiweka kwa muda wa miaka 5 utakuwa na akiba ya million 3.Baada ya hapo anzisha mradi wa milion 3 halafu huo mradi usimamie vizuri kwa muda wa miaka 5 hakika nakuambia baada ya miaka 5 unaweza kuwa na miradi mikubwa zaidi ya 3.

Kisha unaweza kuachana na kuajiriwa ukajikita kufanya shughuli zako ukawaachia vijana wanohitimu chuo nao wapate ajira na kutengeneza mitaji ya kujiletea maendeleo katika maisha yao. Hapa hata ukiipata pension yako utaweza kuitumia vizuri kwa furaha kubwa sana.



Tusing'ang'anie ajira ndugu zangu, mtu mpaka anakuwa mzee tena anapunguza hadi mika eti achelewe kustaafu,hakika huu ni uwezo mdogo wa kufikiria. 

Mpaka natamani kama serikali ingeweka utaratibu wa kupunguza miaka ya kustaaf,badala ya miaka 60 ya lazima ni vizuri 45 ndo ikawa kwa lazima ustaafu. Kwa sasa vijana wanamaliza chuo kikuu na miaka 23 au 22 akifanikiwa kuajiriwa na umri wa 25 basi utastaafu kwa lazima baada ya mika 20 ambayo standard kabisa. Wewe unataka mpaka uzeekee kwenye ajira na vijana watafanyaje?

Mwisho ; fanya ajira kama ni sehemu ya kusaidia kutimiza maono ya .mwenye taasisi na kujipanga kwa ajili ya kuandaa ajira yako .mwenyewe.




Be blessed by:

Lushinge makelemo 

Director of Makelemo consulting services 

0763826410

lmakelemo@yahoo.com makelemoconsultingservices79@gmail.com 


Post a Comment

Previous Post Next Post