Namna ya kukuza biashara yako!



Ili  kuwa na biashara kubwa si lazima uwe na mamilioni ya pesa kama mtaji,bali  inategemea mifumo madhubuti unayoweza kuiweka kwenye biashara yako .


Watu wengi sana wameanza biashara na mitaji mikubwa lakini mwisho wa siku wameishia kufilisika na biashara zao  kufa vibaya sana kwa kutozingatia mifumo mizuri ya uendeshaji wa biashara zao. 

Unaweza kuanza na mtaji hata kuanzia 200,000 mpaka 500,000 ukawa millionaire kwa kufanya udhibiti kama wanaofanya wenye makampuni makubwa hapa duniani.

Mifumo ya kifedha [financial Management] ndo tiba pekee .Lazima uifanye biashara yako ni tofauti kabisa na wewe, chukulia kuwa ofisi yako au duka ni mtu  mwingine kabisa. 

Kosa kubwa wafanyabiashara wanalolifanya ni kuifanya biashara kama ndo yeye mwenyewe hivyo hujkuta akijisikia kuchukua kiasi cha pesa chochote anachota tu bila utaratibu.  Tabia his husababisha kushindwa kutathimini mwenendo wa biashara yako .

Ukianzisha biashara hakikisha unaweka angalau 10% ya kila faida unayoipata katika biashara yako na hii pesa kamwe isiguswe mpaka itakapokuwa kiasi kikubwa kuweza kufungua biashara nyingine au kupanua biashara iliyopo. 

Jitahidi kufanya mahesabu kila wiki au kila mwezi na kufanya ulinganifu na kuweza kuchukua hatua stahiki kunapokuwa na changamoto yoyote katika biashara yako. Pia uweze kujua faida na hasara unayoipata, na kufanya marekebisho panapohitajika.

Pia kama una mtaji wako mwenyewe  usiingiwe na tamaa ya kwenda kukopa  pesa kuongeza kwenye biashara yako, maana tatizo la kuanza biashara kwa mkopo haitaweza kukua kwa wakati au yaweza kufa ndani  ya muda mfupi sana.

Nimeona watu wengi sana wakianzisha biashara zao kwa mikopo wameishia kufilisika na kupata aibu kubwa kwenye Jamii. Mtu anapokopa ili kuanzisha biashara hatakuwa na utulivu katika biashara yake, atakuwa hawazi kukuza biashara bali anawaza  marejesho  ya mkopo tu.

Tena siku hizi kuna aina ya mikopo wanaiita  kausha damu, watu hawa wana riba kubwa sana na unatakiwa kila siku au kila wiki upeleke rejesho je hapo ndugu yangu utatoboa  kweli?

Kuna mtu mmoja mkoa fulani hapa Tanzania anafanya biashara hizi za kukopesha ukichukua  100,000/= kila siku inazaa 10,000/= sasa niambie katika Hali huyo utafaulu? La hasha  si rahisi 

Ushauri  wangu; Anza na kidogo ulichonacho kikuze taratibu  bila haraka mwisho utakuwa mfanyabiashara mkubwa sana bila stress. 
Hakuna raha kubwa duniani ukiishi bila kudaiwa .

Kwa Ushauri zaidi wa kibiashara na fedha wasiliana nasi;
0763 826 410
Lushinge Makelemo 
EMAIL: lmakelemo@yahoo.com 
            mkmconsultingservice@gmail.com

Post a Comment

Previous Post Next Post