Kuajiriwa ni Ile hali ya mtu kufanya KAZI za mtu mwingine kwa malipo/Mshahara, kujiajiri ni Ile hali ya mtu kuamua kufanya kazi zake mwenyewe.
Watu wanaoajiriwa mpaka anafikisha miaka 60 ndo anacha ajira yaani kwa lazima kama hakuweka Mambo sawa wakati wa ajira yake kamwe hataweza kutoboa maisha.
Shida na hasara kubwa ya kuajiriwa ni;
1. Kuuza muda wako kwa mtu kwa malipo yanayoitwa Mshahara.Kwa kipindi tulichonacho Tanzania ni mgumu sana hasa kulingana na soko la ajira, wanafunzi maelfu wanahitimu kozi mbalimbali na kuingia kusaka ajira, mwisho wake wakikosa wako tayari kufanya KAZI ya mshahara hata wa 150000.Ukipiga mahesabu pesa yote inaishia Kula, nauli na pango la nyumba matokeo yake huyu mtumishi anaingia katika madeni makubwa nakujikuta mwsho wa mwezi unapofika anaenda kupokea hewa maana mshahara umeishia wote kwenye madeni.
Na hapa muda wako unadhitiwa na mtu,huwezi kutoka nje ya maeneo ya kazi bila kuwa na ruhusa maalumu.Unapewa siku 28 kwa mwaka zikiwemo na weekend zote kati ya siku 365 za mwaka mzima ili nawe ukapumzike,hata hivyo muda wowote ikitokea dharura waweza kuitwa ofisin hata kama upo likizo ingawa Sheria za kazi haziruhusu kufanya hivyo hii hatari sana.
Yàani unaruhusiwa kufanya mambo yako full time siku 28 tu kwa mwaka na237 unahenyeka kwa mwajiri duh!!
Huyu mtu hapo juu anafanya tu kazi ila basi tu hana mood kabisa.
2. Kuuza uhuru wako, hii ni kama utumwa fulani ingawa hii ni tofauti na utumwa halisi ambao mtu hapewi ujira. Mtu anapokuwa katika ajira wajiri wapo tayari hata kukutukana kwa sababu wanakulipa mwisho wa mwezi.
Swala la kupewa siku 28 tu kwa mwaka kupumzika huu ni utumwa fulani ambao posho yake ni mshahara,Amka mtanzania.
3.Unaamuliwa kiwango Cha kipato mfano katika nchi yetu taasisi nyingi sana za binafis hazifuati kabisa Sheria za kazi mfano unakuta Mtumishi anafanyishwa kazi tangu saa mbili asubuhi mpaka saaa Kumi na mbili jioni hivi kweli huyu mtu ataweza kujishughulisha na mwaswala yake binafisi ya kiuchumi? La hasha hapana.
Lakini ukiwa umejiajiri mwenyewe unaamua wewe mwenyewe utengeneze kiasi Gani cha pesa kwa siku au kwa mwezi.
4.Ukiwa umeajiriwa unatimiza maono ya mwenye taasisi.
Unapokuwa umeajiriwa huwezi kawe kutimiza maono na mipango yako, na ndo maana mwajiri yoyote akiona mtumishi wake ananza kuwa na Maendeleo makubwa anaanza kuchunguzwa sana na kuundiwa tume ya uchunguzi kwa sababu mwajiri anaamini kuwa mshahara alioupanga kamwe hauwezi kukutoa kimaisha ili uendelee kufanya KAZI kwake na ukifika umri wa Miaka 60 wanakutupa nje na unapewa kiinua mgongo ili uende ukafie mbali huko.
Na hapo hujajiandaa vizuri na purukishani za mitaani huchukui round utakufa mapema Sana jamani Mungu mwema azidi kutusaidia Sana.
Mpka natamani kuiomba serikali ya jamhuri ya muungamo wa Tanzania ibadilishe mfumo wa kustaafu ili watumishi wastaafu wastafu na umri wa Miaka 45 ili Ile Miaka 15 ya kuelekea Miaka 60 apigane vita mtaani na kujenga misuli ili asife haraka sana huyo mtu.
Faida kubwa ya kujiajiri au kuwa na kazi Yako mwenyewe ni;
1.Unajiamulia kipato chako na una kuwa na uhuru mkubwa wa kifedha.
Hapa unatakiwa kuwa na juhudi kubwa ili uweze kutengeneza kipato kikubwa.
2. Una huru na muda wako. Hapa unaweza kufanya mambo makubwa sana maana una manage muda wewe mwenyewe na hakuna wakukuingilia.
3. Hapa unaweza kutimiza maono yako kikamilifu.
Asante Sana
Kwa msaada zaida wasiliana nasi kwa
0763 826 410
Whatsapp 0653 552 236
Email address lmakelemo@yahoo.com