Wafanyakazi/wajiriwa ni injini ya taasisi au kampuni

 Kama nilivyozungumza katika makala iliyopita kuwa kuajiriwa ni kufanya kazi za mtu mwingine na kutimiza maono ya mmiliki wa kampuni au taasisi husika 

Leo napenda kuzungumza umuhimu wa kumtunza na kumheshimu mfanyakazi ili aweze kukuzalishia Zaidi na taasisi iweze kuwa imara na endelevu. Mfanyakazi ni injini ya kampuni au taasisi husika,bila kuwa na wafanyakazi huwezi kutimiza maono yako.


Mambo makuu matatu (3) mwajiri akiyafanya hakika kampuni yake itakuwa na ustawi mkubwa na endelevu;



1. Kumthamini na kumpa heshima kubwa mfanyakazi;- Binadamu yoyote hapa duniani anapenda sana kupewa heshima yake, na asipopewa heshima yake kamwe hawezi kufanya majukumu yake kwa moyo . Lakini kwa bahati mbaya wajiri wengi jambo hili hawalijui kama wanalijua basi wanajaribu kuweka pamba masikioni. 

Wafanyakazi wanachukuliwa kama ni watu ambao ni daraja la tatu ambalo ni daraja la chini kabisa. Wajiri wapo tayari kuwatukana na kuwatishia kuwafukuza kazi hata kama mafanyakazi ana haki katika eneo fulani. Hali kama hii huondoa marali ya watumishi katika kazi na kusababisha huduma kudorora na uzalishaji kushuka kwa kiwango kikubwa.

Iwapo watumishi wataheshimiwa na kuthaminiwa watajiona pia wao ni sehemu kubwa ya mafanikio katika kampuni au taasisi.Mfano Mimi niliwahi kufanya kazi katika taasisi Moja hapa Mwanza, nilikuwa meneja na afisa mwajiri (Human resources officer) siku Moja mfanyakazi wetu alijiuzuru ghafla bila notisi ya siku 30, na kwa kuwa taasisi hiyo ilikuwa hospital,na wagonjwa wengi walikuwa wanamsubiri huyo daktari kwa ajili ya huduma tulipata wakati mgumu sana kama uongozi katika jambo hili.Ilibidi kuomba msamaha kwa wateja wetu,na huduma za kitengo hicho ilibidi zifungwe kwa muda fulani ili kutafuta mtaalamu mwingine.

Katika tukio hili nilijifinza jambo kubwa sana kuwa wafanyakazi katika kampuni au taasisi ndo injini halisi viongozi au mmiliki ni kama dereva  tu, maana injini ikinoki gari haliwezi kuondoka kamwe.

Hivyo kumthamini na kumheshimu mtumishi ni jambo la muhimu sana kulizingatia kwa Kila mwajiri ili kuwa na taasisi iliyostawi na endelevu.




2. Kuwalipa vizuri wafanyakazi:

   Jambo la kuwalipa vizuri wafanyakazi ni jambo la muhimu sana kulizingatia kwa sababu mtumishi akiwa Hana msongo wa mawazo ana uwezo mkubwa sana wa kufanya Mambo makubwa katika kampuni au taasisi husika.Kama taasisi yako ina uwezo mkubwa wa kifedha walipe mishahara minono wafanyakazi wako ili wafurahie maisha na wakuzalishie pesa nyingi Zaid, na kama siyo waeleze ukweli kuhusu Hali halisi ya kampuni.Mfano nimewahi kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi katika  hospital Moja mkoa wa Geita kwa kweli nilishangaa sana kuona wale watumishi wanavyothaminiwa na mwajiri wao.

Asubuhi wanapata chai Bure watumishi wote pamoja na chakula Cha mchana pia bure,na mishahara minono.Kwa kweli utendaji kazi wa watumishi wa hospital hiyo ni mzuri sana, wengine hadi ajira za serikali zikitoka hawataki kabisa kuomba hii nikutokana na mazingira mwajiri wao alivyoweka, lakini taasisi zingine zikitoka ajira za serikali Hadi watumishi wanafanya sherehe kama vile wametoka utumwani Misri kwa Farao hii ni hatari sana kwa uhai wa taasisi au kampuni.



3. Kuwashirikisha maono na mipango ya taasisi yako.

  Kwa kuwa Hawa wafanyakazi ni injini ya taasisi au kampuni yako,unapaswa kiwashirikisha maono yako,kwamba unataka ufike wapi katika ustawi wa biashara yako maana wao ndo wanaotekeleza mipango  ya kampuni kutimia. Tatizo kubwa wajiri wengi wanawaona wajiriwa ni kama watu wasio na mchango wowote katika taasisi kimawazo wakati siyo hivyo kabisa.

Mimi Nina uhakika kabisa kuwa wafanyakazi Huwa Wana mawazo mazuri sana ya kuipeleka mbele taasisi au kampuni, laiti wangesikilizwa mambo makubwa yangefanyika katika biashara husika.Kuna wakati mwingine watumishi wanaweza kuwa na mawazo mazuri sana kushinda hata kiongozi.

Kwa hiyo ikiwa taasisi yoyote ikifuata Mambo haya matatu;

Kuwathamini wafanyakazi,

Kuwalipa vizuri na kuwashirikisha maono yako na mipango hakika kampuni au taasisi yako itastawi kwa spidi kubwa sana,kwa kuzingatia haya unaweza kuwa na safari ya Miaka 10 ikafupishwa ikawa mwaka mmoja tu hii inawezekana kabisa.


Kwa ushauri zaidi na namna tunavyoendesha mafunzo na semina kwa viongozi na watumishi  ili  kuleta matokeo makubwa ,wasiliana nasi kwa namba zifuatazo

Makelemo consulting services

Mwanza

+255 763 826 410

Whatsapp;+255 653 552 236

Email: lmakelemo@yahoo.com

mkmconsultingservice@gmail.com 

Website: www.makeconservices.com







Post a Comment

Previous Post Next Post