Watanzania wengi wamekuwa wakitamani sana kukimbilia nchi za nje kwa ajili ya kutafuta maisha et Tanzania hakuna maisha.
Mimi napingana na mtazamo huu kabisa kwani Tanzania ina kila fursa ambazo unaweza usizipate katika nchi zingine. Watu wengi ambao wangezitumia fursa hizi wasingetamani kwenda ulaya kuishi kama watumwa kwa mabosi wa huko.
Mfano mtu aliyetakiwa kusafirisha( export ) mazao Ulaya anaenda ulaya kuzoa uchafu na kuosha magari eti sifa kwamba yupo Ulaya hii ni huzuni kubwa sana kwa Taifa.
"I shall become millionaire in the same Tanzania people are running away to Europe "
Kuna fursa kuu mbili ambazo kama mtanzania akizitumia vizuri bila kisingizio cha viongozi wa serikali anaweza kuwa milionea ndani ya muda mfupi sana. Angalia hapa chini::
- Kilimo: Nchi nyingi duniani hapa Tanzania ni mojawapo ya nchi iliyo na aridhi kubwa sana na ambayo haijatumika. Tanzania inaweza kulisha bara la Ulaya bila shida yoyote. Wakati Ulaya wanakuja kutafuta malighafi Tanzania halafu watanzania wanakimbilia Ulaya kutafuta maisha really this is sad. Ukijikita katika kilimo na kushirikisha wataalamu katika mipango yako ya kilimo rafiki yangu, yaani utatoboa vizuri mno kwani kila binadamu anahitaji kula.Kama biashara ya kudorora hapa duniani biashara ya chakula ndiyo itakuwa ya mwisho kudorora na wakati huo binadamu watakuwa wameisha duniani.