Biashara nyingi Huwa zinakufa kwa sababu ya kukosa miongozo thabiti ya kifedha ( Strong financial management). Kwani biashara yoyote pesa isipowekewa utaratibu mgumu wa kutoka au kutolewa itapelekea watu kujichukulia tu pesa bila mpangilio maalumu.Mfano Mtumishi au hata kiongozi wa taasisi kukiwa na uhitaji wa pesa halafu anamwagiza tu mhasibu atoe pesa bila hata maandishi hii utajikuta mapato na matumizi hayaeleweki kabisa.
Faida ya kuwa na Sera nzuri ya miongozo ya fedha katika kampuni au taasisi ni kama ifuatavyo;
1. Kudhibiti matumizi ya taasisi.
Kamwe huwezi kudhibiti matumizi kama hakuna mwongozo maalumu uliowekwa katika kampuni au taasisi.ili uweze kudhibiti matumizi lazima uwekwe utaratibu mgumu namna ya kuomba pesa yaani inabidi uwepo mchakato ( process) wa kupata pasa kwenye taasisi. Mfano mtumishi anapoomba pesa kwa ajili ya matumizi ya kampuni au taasisi, lazima ajaze fomu ya maombi (request form) na hii fomu inapita kwenye mikono angalau ya watu watatu kwa ajili ya kuidhinisha matumizi husika.
2. Kujua mapato ya taasisi au kampuni.
Kama hakuna mfumo wa kifedha katika biashara yoyote pesa hazitajulikana zinazoingia na kutoka.Pia ni vigumu sana kupima ukuaji halisi wa biashara.
Zipo faida nyingi sana za kuwa na mfumo thabiti wa sera ya utawala wa fedha hizi ni baadhi tu.
Asante Rafiki yangu kwa kusoma makala hii itakusaidia sana kwa sehemu;
By Lushinge Makelemo
Director
Makelemo consulting services
Mwanza