Njia tatu 3 za kuwafanya watumishi katika taasisi yako kujiaikia umiliki wa taasisi ili walete matokeo makubwa katika utendaji wa kazi.

 



Habari za leo ndugu masomaji, katika siku ya leo napenda kukufahamisha kuwa katika taasisi yoyote watu wote ni wa muhimu sana ila mtumishi ni wa muhimu zaidi kwa sababu huyu ndiye aliye mstari wa mbele katika  kuinua au kuua taasisi.

Wajiri wengi wamekuwa wakiwachukulia kawaida sana waajiriwa kana kwamba hawana maana yoyote au hwana mchango wowote,ni kama watu ambao hawana sehemu ya kwenda, na hii inapelekea kuwanyanyasa na kushindwa kuwapa haki zao stahiki.

Kwa Hali hii ndo maana wajiriwa wengi hawana ule moyo wa kuwaza kuwa pindi wawapo kwenye taasisi au kampuni fulani ni mali Yao; maana ndipo pale wanapata pesa kwa ajili ya kutimiza mahitaji yao muhimu.

Watumishi wengi wanakuwa na lugha ya "Mimi nasubiria mshahara wangu tu mwisho wa mwezi watajijua wenyewe" haya yote yanasababishwa na uongozi uliowekwa pamoja na mmiliki mwenyewe. Kwa hiyo mambo matatu yafuatayo kampuni au taasisi yoyote ikiyafanya kwa Mtumishi hakika itakuwa na matokeo makubwa sana ambayo ni chanya na taasisi kufa na ndiyo;

1.  Kuwashirikisha wafanyakazi mawazo yako;

      Jambo hili ni la muhimu sana kwa kweli,mtu yoyote hapa duniani anapenda kuhisi kuwa anathaminiwa na mtu mwingine ili naye aweze kuwa wazi moyo wake.Mfano: Mtu ambaye ni mkubwa pia amekuzidi umri au kimadaraka akija kukuomba ushauri au kukupa mawazo ili msaidiane kutatua changamoto fulani je utajisikiaje? Hakika utajisikia vizuri sana na hapo unaweza kuhisi kama kichwa kimekuwa kikubwa sana.pia utajisikia hamasa sana ya kufanya kazi kwa bidii zaida. 

Lakini tatizo kubwa lililopo kwa wamiliki wengi wa makampuni na taasisi mbalimbali ni kuwadharau tu wafanyakazi na kuwachukulia kama daraja la chini sana kama watu wasio na heshimu kama vile watumwa ambao hawatakiwi kusikilizwa.Matokeo yake hakuna matokeo makubwa yanayoweza kutokea.

Mfano Mimi niliwahi kuwa na cheo kikubwa sana, nilikuwa afisa mwajiri, afisa utawla na katibu wa bodi ya wadhamini katika Ile taasisi(Hospital) nilijitahidi sana kuwa naita Mtumishi mmoja mmoja kwa taaluma yake na kumtia moyo na kuomba mawazo kutoka kwake namna ya kufanikiwa  kwa hospital yatu.

Pia wakati wa vikao vya Kila asubuhi nikiwatia moyo wafanyakazi na kuomba mawazo Yao juu ya kuwa na mafanikio.Kwa kweli watu walipata moyo sana na walifanya kazi kwa moyo sana na hospital ilipata sifa kubwa sana hapa Mwanza mpaka ikawa tishio kwa hospitali zingine za jiji la Mwanza.

2. Kuwashirikisha wafanyakazi maono ya kampuni au taasisi.

Kuwashirikisha wafanyakazi maono ya kampuni au taasisi yako ni muhimu sana maana watumishi lazima wajue dira na dhima ya kampuni au taasisi wanyofanyia kazi ili nao wawaze namna Gani ya kutoa mchango wao maana wafanyakazi ndiyo wahusika wakubwa wakutimiza maono ya mwajiri.Hakika huwezi kutimiza maono yako bila kuwa na wasaidizi kamwe huwezi ndugu, maana hata Mungu ana wasaidizi wake kama vile malaika,Yesu Kristo na wanadamu pia.

Iwapo utajenga utamaduni wa kuwashirikisha maono na mipango yako wafanyakazi hakika utafika mbali sana kimaendelo.mfanyakazi moyo wake ukifunguka vizuri kabisa anweza kukufanyia KAZI nzuri sana mpaka ukasahangaa . Tatizo kubwa lililopo kwa wamiliki wengi na hasa viongozi walikabidhiwa madaraka kutothamini wafanyakazi bila kujua watumishi ndo UTI wa mgongo wa kampuni au taasisi.

3. Kuwathamini wafanyakazi kwa  kufuata miongozo iliyowekwa na kampun au serikali.

Kila taasisi Huwa ina miongozo yake lakini mwongozo mama ni labor law, Sheria za kazi, hata kama taasisi itakuwa na mwongozo wa ndani lazima uzingatie haki na utu wa mfanyakazi.

Iwapo kampuni au taasisi itazingatia haya hakika itasonga mbele kwa spid ya haraka sana .

Nawatakia siku njema wasomaji wangu.

By Lushinge Makelemo

Director

 Makelemo consulting services.

Mwanza 


Post a Comment

Previous Post Next Post