Katika biashara yoyote hapa duniani,ili uweze kufanikiwa lazima uwe na mipango madhubuti na mbinu kabambe ili kuweza kutawala soko. Ni muhimu sana kutumia mbinu sahihi ili kufanikiwa katika biashara yako Watu wengi husingizia nguvu za shetani zinazopelekea biashara zao kufa, wakati si kweli kabisa.
Watu wengi sana wamefilisika kwa sababu ya kutokuwa na mbinu imara za kufanya katika biashara zao. Waganga wa kienyeji ni wajanja sana ndugu yangu anaweza kukupa masharti kwenye dawa zake utekeleze kumbe ni mbinu zake apate naye kipato.
Mfano: Kijana mmoja mkoa fulani hapa Tanzania, alikuwa na biashara ya duka la chakula mauzo yake yalikuwa kidogo sana hatimaye duka lake likaporomoka vibaya sana mpaka akaelekea kufilisika kabisa. Akapata wazo la kwenda kwa fundi au mganga wa kienyeji, mganga akampatia dawa kwa ajili ya biashara yake kwa masharti yafuatayo:
- Akamwambia hiyo dawa lazima kila siku aitumie kwa kujifukiza kabla ya kuanza kuuza bidhaa asubuhi.Na ilikuwa lazima afike dukani kabla ya saa moja asubuhi yaani jua halitakiwi lichomoze akiwa nyumbani,na kama ikitokea hivyo basi hatakiwi siku hiyo kufungua duka.
- Ndani ya mwaka mzima hatakiwi kutumia mapato ya dukani kuhonga mwanamke yoyote wala kunywa pombe.
- Ndani ya mwaka mzima hatakiwi kula kwa mama lishe au mama ntilie na kama angekula angefilisika mara moja.
Hebu tuangalie baada ya mwaka mmoja:
Huyu kijana baada ya mwaka mmoja alienda kuangalia kwenye bank akaunti yake alikuwa na 50millioni huwezi amini. Unadhani dawa kweli ndo ilifanya kazi? La hasha yule mganga alikuwa na akili Sana aisee! Maana sharti la kwanza wengi sana wanashindwa kutekeleza unakuta mtu analala mpaka saa mbali ndo anaamka kwenda kufungua duka hii ni hatari sana, maana hata maandiko kwenye biblia kwa wakristo inasema apendaye usikingizi atakuwa masikini.Maana unapofungua saa 2 asubuhi tayari wengine wameshauza vya kutosha.
Pia kwa sharti la pili, ndugu yangu kama shimo la pesa zinakozama na kufilisika kwa biashara nyingi ni kupenda sana wanawake; na mwanamke wa siku hizi akikupata lazima afanye la maana kwako kuhakikisha pesa inahamia kwake na usipokuwa makini waweza kufa kama mtumwa hapa duniani. Wanaume wengi wamekufa bila kutimiza ndoto zao za utajiri kwa sababu ya kumaliza pesa zao za biashara katika kuhonga wanawake hii ni huzuni kubwa Sana.pia pombe ina maliza sana pesa.
Sharti la tatu kutokula kwa mama ntilie au hotelini.katika sehemu pia inayomaliza pesa kwa wafanyabiashara wengi ni kula hotelini utakuta faida nyingi inatumika kwenye chakula cha hotelini. Lakini kama ukiweza kubeba chakula kutoka nyumbani utaokoa pesa nyingi Sana.
Kwa hiyo huyu jamaa alipotimiza masharti haya ndani ya mwaka mmoja alifanikiwa sana kibiashara kupita maelezo. Pia na wewe unaweza kufanya kama alivyofanya huyo kijana ukafanikiwa ndani ya muda mfupi.
Hebu tuangalie baadhi ya mbinu muhimu katika kufanikiwa kwenye biashara:l
- Uelewa wa Soko:
Tafiti za kina: Fanya utafiti wa kina kuhusu aina mbalimbali za bidhaa zako zinazopendwa, bei za kawaida, na washindani wako.
Utambulishe wateja wako: Elewa ni aina gani ya watu wananunua bidhaa zako, maslahi yao, na mahitaji yao.
Fuatilia mtindo: Jiweke katika hali ya kujua mitindo mipya na mabadiliko katika tasnia ya bidhaa zako.
- Ubunifu wa kupangilia bidhaa zako:
Weka bidhaa zako katika hali juu:Tumia vifaa vya ubora wa hali ya juu katika utengenezaji wa biashara yako.
Utofauti wa bidhaa: Toa aina mbalimbali za bidhaa ili kukidhi mahitaji ya wateja tofauti.
- Uuzaji na Masoko:
Uuzaji wa mtandaoni: Tumia mitandao ya kijamii, tovuti yako mwenyewe, na majukwaa mengine ya e-commerce kuuza bidhaa zako.
Masoko ya kimwili: Shiriki katika maonyesho, soko la mboga, na matukio mengine ya ndani.
Uhusiano na wateja: Jenga uhusiano mzuri na wateja wako kwa kujibu maswali yao haraka na kutoa huduma bora baada ya mauzo.
- Ufungashaji na Uwasilishaji:
Ufungashaji wa kuvutia: Paki bidhaa zako kwa njia ya kuvutia na salama.
- Usimamizi wa Fedha:
Bajeti: Tengeneza bajeti na ufuatilie gharama zako kwa makini Sana.
Bei: Weka bei zinazofaa kwa bidhaa zako.
Uhasibu: Weka kumbukumbu za kifedha kwa usahihi.
Mbinu zingine:
Ushirikiano:Shirikiana na wabunifu, na wafanyabiashara wengine.
Masomo endelevu: Endelea kujifunza kuhusu mbinu mpya za biashara na mitindo ya soko.
Kumbuka: Kufanikiwa katika biashara yoyote kunahitaji uvumilivu, bidii, na ubunifu. Kwa kutumia mbinu hizi na kuendelea kujifunza, unaweza kujenga biashara yako yenye mafanikio makubwa Sana.
Je, ungependa kujua zaidi kuhusu mada mahususi katika biashara? Kwa mfano, unaweza kuuliza kuhusu:
Jinsi ya kupata wateja wapya
Mbinu za kutangaza bodi zako kwenye mitandao ya kijamii
Na mengine mengi
Tafadhali usisite kuuliza!
Stay blessed
Lushinge Makelemo
Business consultant
+255 763 836 410
Email address: mkmconsultingservice@gmail.com