HUWEZI KUIBADILISHA JANA ILA UNAWEZA KUBADILISHA KESHO YAKO

 



Huwezi kamwe  kuibadilisha jana,  hatuwezi kurekebisha yaliyopita, tuna uwezo mkubwa wa kuunda siku zetu zijazo na kutengeneza hatma nzuri ya maisha yetu.

Jana imepita:  Yote yaliyotokea jana ni historia na hatuwezi kuyarudisha. Kunung'unika au kujutia hakutabadilisha chochote.

Kesho ndiyo iko mkononi mwetu:  Tuna uwezo wa kuchagua matendo yetu, mawazo yetu, na mwelekeo wa maisha yetu.

Mabadiliko yanawezekana: Tunaweza kujifunza kutoka kwa makosa ya jana na kutumia maarifa hayo kuboresha kesho yetu.

Jinsi ya kubadili maisha yako;

Kubali makosa:  Badala ya kujilaumu kwa makosa ya zamani, tumia kama fursa kujifunza na kukua kwa maana muda unaotumia kujilaimu au kuwalaumu wengine kama ndo chanzo cha kushindwa kwako, tumia muda huo kufanya tathimini ya kina kuhusu hatma yako.

Weka malengo:  Fafanua unachotaka kufikia katika maisha yako na tengeneza mpango wa kuyafikia.

Chukua hatua: Usisubiri fursa, bali chukua hatua za kuunda maisha unayoyataka.

Uwe na mtazamo chanya:  Mtazamo mzuri unakusaidia kushinda changamoto na kufikia malengo yako.


Mfano:


Tuseme umefanya mtihani na hukufanya vizuri kama ulivyotarajia. Badala ya kujipa moyo, unaweza kutumia msemo huu kukukumbusha kwamba unaweza kuboresha matokeo yako katika mtihani ujao kwa kujisomea kwa bidii zaidi na kuomba msaada kutoka kwa mwalimu wako.


Kwa kauli, hii tunapaswa kuwa na nguvu ya  kutuhimiza kuishi maisha yenye maana zaidi. Tunapaswa kuacha kuangalia nyuma na badala yake tuangalie mbele kwa matumaini na matarajio.

Kumbuka kujutia ya nyuma hakutabasilisha chochote zaidi ya kukupotezea wakati tu.

Stay blessed 

Lushinge Makelemo 

mkmconsultingservice@gmail.com 

+255763826410

Post a Comment

Previous Post Next Post